Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba hii leo amekutana na
kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Finland.
Katika mazungumzo yao
yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Dar es Salaam, wabunge
hao wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inazofanya za kulinda na
kuhifadhi mazingira.
Awali, akiwakaribisha
wabunge hao Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano mzuri uliopo
baina ya Tanzania na Finland na kuwashukuru
wabunge hao kwa kufanya ziara hiyo ya kikazi nchini Tanzania.
Waziri Makamba
amesema Serikali ya awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuimarisha Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa Mkakati Mkubwa wa Kitaifa wa
kupanda miti nchi nzima hususan maeneo kame ili kunusuru nchi na athari za
mabadiliko ya Tabianchi.
“Hivi sasa tuko
katika hatua za kuainisha maeneo yatakayopandwa miti hiyo kwa kuangalia aina za
udongo na miti itakayoweza kuhimili katika maeneo husika” Alisisitiza Makamba.
Waziri Makamba
ameiomba Serikali ya Finland kuendelea kushirikiana zaidi na Serikali ya
Tanzania ili kufikia malengo endelevu ya Uchumi na maendeleo ya Viwanda bila
kuathiri Mazingira.
Naye Balozi wa
Finland Nchini Tanzania Bw Mart Akhtsary aliyeambatana na ujumbe wa wabunge
kutoka Finland amemhakikishia Waziri Makamba kuendeleza na kudumisha
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment