TANGAZO


Sunday, April 10, 2016

Waliolipua Brussels walikuwa wamelenga Paris


Image copyrightEPA
Image captionWaliolipua Brussels walikuwa wamelenga Paris

Wavamizi wa kujitolea muhanga walioishambulia mji mkuu wa Ubelgiji , Brussels mwezi uliopita walikuwa wanalenga kuishambulia upya Ufaransa.
Kiongozi wa upelelezi anasema kuwa kundi hilo liliamua kuishambulia Brussels baada ya kuhofia kukamatwa na polisi waliokuwa wakifanya upelelezi kwa kasi na kufuatiia nyendo zao.
Afisi ya kiongozi wa mashtaka mjini Brussels tayari wameshafichua uhusiano baina ya washambuliaji hao wa Brussles na wale waliotekeleza mashambulizi mjini Paris Ufaransa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Shambulizi lilisababisha vifo vya watu 130.
Aidha wamethibitisha kumfungulia mashtaka mshukiwa mkuu wa mashambulizi hayo bwana Mohammed Abrini, ambaye alihusika katika shambulizi la Brussels na vilevile lile la Paris.

Image copyrightEPA
Image captionWavamizi wa kujitolea muhanga walioishambulia mji mkuu wa Ubelgiji , Brussels mwezi uliopita walikuwa wanalenga kuishambulia upya Ufaransa.

Hayo yanajiri baada ya upande wa mashtaka kutangaza kuwa wamemkamata mshukiwa wa mashambulizi ya Ubelgiji aliyekuwa na kofia aliyekuwa anatafutwa.
Mshukiwa huyo alinaswa na kamera fiche akiwa na walipuaji wa kujitolea muhanga lakini akatoweka baada ya ukanda wake uliojaa vilipuzi kukosa kulipuka.
Viongozi wa mashtaka walisema kuwa Mohamed Abrini alikiri kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtu wa tatu aliyeonekana kwenye picha za CCTV akisukuma troli ya mizigo.

Image copyrightAP
Image captionMohammed Abrini, ambaye alihusika katika shambulizi la Brussels na vilevile lile la Paris.

Yeye ni mmoja wa watu wanne walioshtakiwa na polisi wa Ubelgiji hiyo jana kwa kushiriki katika milipuko iliyotokea kwenye uwanja wa ndege na njia ya chini kwa chini ya treni.
Yeye pia ameshirikishwa na mashambulizi ya Paris ya Novemba mwaka uliopita yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Mwingine aliyeshtakiwa ni raia wa Sweden Osama Krayen, ambaye ametambuliwa kama mtu aliyeonekana akuzungumza na mshambulizi wa kujitoa mhanga katika mtandao wa treni wa Malbeek muda mfupi kabla ya shambulio.

No comments:

Post a Comment