Pigano la marudio kati ya Tyson Fury na Wladmir Klitschko litaandaliwa mjini Manchester mnamo mwezi Julai tarehe 9 kulingana na mkufunzi wa bondia huyo wa Uingereza.
Peter Fury alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter siku ya Ijumaa na tanagazo jingine linatarajiwa baadaye.
Fury ambaye ni mzaliwa wa mjini Manchester na ambaye ana umri wa miaka 27,alimshinda raia wa Ukraine Klitschko kwa pointi mjini Dusseldorf mwezi Novemba ili kushinda mikanda mitatu ya WBA,IBF na WBO.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Fury ni Muingereza wa tano kushinda mataji hayo ya uzani mzito zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment