
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimia wananchi wa Mkoa wa Katavi alipowasili katika mkoa huo jana kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima.(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo, Katavi)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Katavi alipowasili katika ofisi za mkoa huo na badae kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Waziri mwenye dhamana na sekta hizo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) alipofanya kikao nao jana mkoani hapo na kuahidi kutatua baadhi ya kero zinazowakabili.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikagua iPad kabla ya kumkabidhi Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima iPad nne kwa ajili ya maafisa habari waliopo katika Mkoa wa Katavi na Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima
akifurahi na kumpa mkono Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya
kupokea iPad nne kwa ajili ya maafisa habari waliopo katika Mkoa wa Katavi na
Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Na Genofeva Matemu-Maelezo, Katavi 05/04/2016
TAASISI za serikali zimetakiwa
kuwashirikisha maafisa habari waliopo katika taasisi zao katika vikao vya maamuzi
ili waweze kua na taarifa na kufahamu maamuzi ya michakato inayoendelea hivyo
kupata nguvu na uelewa mzuri wa kwenda kueleza umma pale wanapotakiwa kutolea
ufafanuzi.
Kauli hiyo imetolewa
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa
ziara yake jana katika Mkoa wa Katavi kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia
pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa Mkoa huo na kutembelea
mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Aidha Mhe. Nnauye
amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na
taratibu kwani serikali inawajali na kuwathamini kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
kuelimisha jamii.
Aidha Mhe. Nnauye amewaomba
watu wa TCRA kusimamia vizuri maudhui ya Radio na Television kwa kuwa wakali na kuacha kucheka na watu ambao wanaweza
kutumia vibaya mabadiliko ya sayansi na
teknolojia kuwaga jamii yetu kidini, kikabila, kikanda na rangi kwa kufanya
matangazo ya kuligawa taifa letu.




No comments:
Post a Comment