Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Rukwa jana wakati wa ziara yake mkoani humo kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa CCM Rukwa Bw. Hypolitus Matete.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kushoto) akuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipofika ofisini kwake wakati wa ziara ya kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizugumza na watendaji kutoka Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokutana nao jana Mkoani hapo kujadili mambo mbalimbali katika sekta hizo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano.
Baadhi ya watendaji kutoka Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofanya ziara yake jana Mkoani Rukwa kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa.
Mwamuzi na Mkufunzi wa mchezo wa netibali Mkoa wa Rukwa Bibi. Louisa Monji akichangia wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya ziara katika mkoa huo jana kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiikagua iPad kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kushoto) kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi kwa maafisa mawasiliano waliopo Mkoani hapo. Mhe. Nnauye alikabidhi iPad tatu kwa Mkoa wa Rukwa jana baada ya kufanya ziara fupi na kuonana na wadau wa sekta anazozisimamia.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta akitoa taarifa fupi kuhusu sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Waziri wa sekta hizo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya ziara Wilayani hapo jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza moja kwa moja
kupitia radio ya Wilaya Nkasi FM alipofanya ziara katika radio hiyo kuona
mafanikio yaliyoletwa na Wilaya ya Nkasi kwa kuwa na radio ya Wilaya.
Na Genofeva Matemu –
Maelezo, Rukwa
05/04/2016
SERIKALI imeamua
kuwekeza kwenye mikoa ya pembezoni kuhakikisha usikivu wa shirika la utangazaji
la taifa unakua mkubwa na wakutosha kwa kuweza kusikika katika maeneo yote
nchini.
Ili kutimiza lengo
hilo Mhe. Nnauye amehaidi kufanya maamuzi magumu kwa kusimamia ubadilishaji wa
baadhi ya vifaa, kuhamishia mitambo maeneo ya milimani pamoja na kuweka busta
zenye nguvu zitakazoweza kufikisha matangazo ya redio na televisheni ya taifa
nchi nzima.
Akitoa taarifa kuhusu
usikivu wa shirika la utangazaji la taifa Mkoa wa Rukwa Kaimu Mkuu wa Kanda TBC
nyanda za juu kusini Bw. Hosea Cheyo amesema kuwa usikivu wa shirika la
utangazaji la taifa upo kwa asilimia sabini na tano tu hivyo kuiomba serikali
kuhamisha mtambo wa shirika hilo katika mlima wa king’ombe ili wananchi wa Mkoa
wa Rukwa waweze kupata fursa ya kusikiliza radio ya taifa.









No comments:
Post a Comment