Mkuu
waMkoawaSimiyuambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw. Anthony Mtaka akizungumza jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya
10 ya Eastern junior Championship katika riadha yanayofanyika katika Uwanja waTaifa jijini
Dar es Salaam tarehe 29-30 April 2016. Wengine pichani ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel (wa pili kulia), Rais wa Shirikisho la Riadha Kenya, Generali mstaafu
Jackson Tuwei (wa tatu kulia) na Dk. Eng Siddig Ibrahim kutoka Sudan.
KatibuMkuuWizarayaHabari,Utamaduni,SanaanaMichezoProf.Elisante
Ole Gabriel akiongea wakati wa ufunguzi wa michuano ya Riadha ya 10 ya East Africa Junior
Championship. Prof. Elisante alitoa ombi kwa wadau mbalimbali kuunga mkono shughuli za riadha kwani ni mchezo rahisi kuwekeza. Kulia kwake ni Rais wa Shirikisho
la riadha Kenya, Generali mstaafu Jackson Tuwei na Dk. Eng. Siddig Ibrahim kutoka Sudan.
Timu
ya washiriki kutoka Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi Prof. Elisante Ole Gabriel
ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupopichani),kabla ya kuanza kwa mashindnao ya Riadha ya
10 ya East Africa Junior Championship yanayofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Riadha Kenya, Generali mstaafu Jackson
Tuwei akizungumza kabla hajamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel (kulia). Bw. Tuwei alisisitiza kufanya michezo ya mara kwa mara ili kujenga umoja na mshikamano katika eneo
la Afrika Mashariki.
Washindi wa mita mia kutoka
Zanzibar, Ally Hamis Gulam (mshindi wa kwanza) na Hassan Hamis (mshindi wa pili), wakinyanyua bendera kuashiria ushindi wao katika michuano ya Riadhaya
10 ya East Africa Junior Championship.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mchezo wa Kurusha Mkuki (Javelin), kutoka
Uganda na Tanzania katika mashindano ya Riadha ya 10 ya East Africa Junior
Championship.



No comments:
Post a Comment