Kiongozi mkuu wa Kanisa la Kianglikana duniani, ametangaza kuwa babaake mzazi ambaye alikuwa anamfahamu sio yeye.
Askofu huyo wa Cantebury, Justin Welby, amesema alifahamu mwezi uliopita kuwa babake mzazi alikuwa balozi wa Uingereza Sir Anthony Montague Browne, ambaye alifariki miaka mitatu iliyopita na wakati mmoja alihudumu kama msaidizi wa Sir Winston Churchil.
Askofu huyo alikuwa akidhani Gavin Welby ambaye alifariki mwaka wa sabini na saba alikwa babake.
Justin Welby ametaja habari hizo kama za kushangaza na alifanya majaribio ya DNA baada ya kupata habari hizo kutoka kwa gazeti moja nchini Uingereza.
Matokeo yake yalifananishwa na yale yaliyopatikana katika nywele za babake.
No comments:
Post a Comment