Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria wakisalimiana huku wakielekea katika Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), jijini Dar es Salaam kwenye ziara ya kutembelea mamlaka hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Sarah Kibonde Msika akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria walipofika kutembelea ofisi za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Antony
Mavunde akieleza jambo wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ziara ya Kamati ya Bunge ilipotembelea ofisi za SSRA. Kamati hiyo inaongozwa na Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (pili kulia).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Antony Mavunde akieleza jambo wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ziara ya Kamati ya Bunge ilipotembelea ofisi za SSRA. Kamati hiyo inaongozwa na Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (pili kulia).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge
Kudumu wakitembelea vitengo mbalimbali ndani ya ofisi za SSRA.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka (watatu kushoto), akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria, walipotembelea mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka akitoa mada na maelezo mbalimbali kuhusu Mamlaka pamoja na Sekta nzima kwa wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea ofisi za SSRA, Dar es Salaam hivi karibuni.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakiwa na uongozi wa
SSRA pamoja na viongozi toka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu),
wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za SSRA.
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Mh. Mohamed Omary Mchengerwa (aliyekaa watatu kushoto), akifuatiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu), Mhe. Antony Mavunde. Kati ya waliosimama ni Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Bw. Juma Muhimbi (wanne kulia), akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka
(kushoto) pamoja na Menejimenti ya SSRA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), akihojiwa na waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari baada ya kikao kilichofanyika wakati Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea mamlaka hiyo.

No comments:
Post a Comment