Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum) alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo Bungeni leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Silafu Jumbe Maufi (Mbunge Viti Maalum) akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali iatamaliza tatizo la upungufu wa vifaa vya kufundishia somo la TEHAMA na walimu wa masomo hayo katika mkoa wa Rukwa.
Wabunge wakiwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla akielekea katika ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO, Dodoma
SERIKALI itaendelea
kutekeleza ahadi zake ilizoahidi ya kuwapatia maji wananchi wake ikiwemo wakazi
wa jiji la Dar es salaam ili kutatua adha ya maji inawakabili katika maenneo
yao.
Kauli hiyo imetolewa
leo Bungeni mjini na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack
Kamwela wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Ubungo jijini Dar es
salaam Saed Kubenea lenye vipengele (a), (b), na (c) lililohoji ni lini
Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.
Mahandisi Kamwela
amesema kuwa Serikali imekamilika na kufanikisha upatikanaji wa maji katika
jiji la Dar es salaam kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mtambo wa Ruvu
Chini na ulazaji wa bomba kubwa lenye kipenyo cha mm 1800 kutoka Ruvu Chini
hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 56.
“Hali ya upatikanaji
wa maji katika jiji la Dar es salaam inaendelea kuimarika kwa kuzingatia
kuongzeka kwa uzalishaji maji kutoka Ruvu Chini ambao una uwezo wa kuzalisha
lita milioni 270 za maji kutoka lita milioni 180 za awali kwa siku” alisema Mahandisi
Kamwela.
Katika kuhakikisha
jiji hilo linakuwa na maji ya kutosha kwa wakazi wake, Mahandisi Kamwela
amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu nao umekamilika na una uwezo wa kutoa
maji lita milioni 196 kutoka lita milioni 82 za awali kwa siku.
Ili kuhakikisha maji
yanawafikia walengwa, Mahandisi Kamwela kazi za ulazaji za ulazaji wa mabomba
mawili kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tenki jipya la maji eneo la
Kibamba na ukarabati wa matenki ya Kimara zimefikia wastani wa asilimia 98,
hatua hiyo imewezesha majaribio ya uendeshaji wa mitambo hiyo kuanza mapema
Aprili mwaka huu.
Aidha, Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali
inaendelea kutekeleza mradi wa Kimbiji na Mpera
ambapo hadi sasa mkandarasi amekamilisha uchimbaji wa visima tisa kati
ya visima 20 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu,
hadi kukamilika visima hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni
260 kwa siku.
Hadi sasa uzalishaji
wa maji katika jiji hilo umefikia lita milioni 390 kwa siku ikilinganishwa na
mahitaji ya lita milioni 450 ya sasa.
Akijibu swali la
nyongeza la Kubenea alioitaka kujua maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ya
maji, Mhandisi Kamwela ameyataja maeneo hayo
yatakayonufaika ni pamoja na maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba,
Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.
Maeneo mengine
yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo,
Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani,
Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati
Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba,
Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.
Kukamilika kwa miradi
yote itaongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam
hadi kufikia lita milioni 750 ambayo yatakidhi mahitaji ya wakazi hao hadi
kufikia mwaka 2032.










No comments:
Post a Comment