TANGAZO


Tuesday, April 12, 2016

FAO JIPYA LA WOTE SCHEME LA PPF LITASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA WATANZANIA

Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akizungumza wakati wa semina hiyo.

FAO jipya la Wote Scheme ambalo ni mfumo wa hiari kwa wanachama ulioanzishwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF utasaidia kuwapa fursa watanzania waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta hizo katika kukuza uchumi.


Fao hilo pia linatoa fursa kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.


Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa alisema hayo juzi wakati semina kwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto mkoani Tanga uliokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu ya mafao yanayopatikana kupitia mfuko huo.

Washiriki wa semina hiyo Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni, Pwani na Tanga, Zahra Kayugwa
Alisema kupitia fao hilo mwanachama anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka mzima bure.


Aidha alisema kupitia skimu hiyo mpya ya mfuko huo unachangia na kuwapa uelewa watanzania utamaduni wa kujiwekea akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati wanapokuwa wakifikia umri wa kustaafu.


 “Lakini pia sisi kama PPF tunarahisisha uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.


Hata hivyo alisema kuwa wanaendelea kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha na utandawazi.


“Fao hili lilianzishwa mwezi wa saba mwaka jana ambapo mwanachama anafaidika na huduma za afya (Kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini - NHIF),mikopo mbalimbali na Fao la Uzeeni(Pensheni) "Alisema Meneja huyo.

Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote Scheme (mfumo wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.
(Picha na Stori kwa Hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:

Post a Comment