Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine, akizungumza na wadau wa mpira nchini kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni ya StarTimes kwa lengo la kumkaribisha Balozi wa StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kutoka nchini Nigeria
Balozi wa StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu akizungumza na wadau wa mpira nchini kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni ya StarTimes kwa lengo la kumkaribisha nchini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
KATIBU Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameishukuru Kampuni
ya StarTimes Tanzania kwa kuthamini soka kwa kumleta nchini mchezaji nguli wa
kimataifa wa Nigeria, Nwanko Kanu.
Mwesiga aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam kwenye hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa na Kampuni ya StarTimes kwa lengo la kumkaribisha Balozi wa
StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kutoka nchini Nigeria.
“Kupitia StarTimes tutaboresha mpira wetu kwa
kuangalia ligi mbalimbali za mataifa ya Ujerumani, Italia na Ufaransa” alisema Mwesigwa.
Ujio wa Kanu nchini ni
fursa na unamanufaa makubwa kwa mustakabali wa ukuaji wa soka hasa kwa
kuzingatia afya ya vijana katika michezo.
Kwa upande wake Balozi
wa StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu ambaye alikuwa mshambuliaji wa Timu ya
Taifa ya Nigeria (Super Eagles) amesema kuwa amekuja Tanzania kwa mwaliko wa StarTimes
na kuahidi kurudi kwa shughuli zake za kimichezo maana amefurahishwa na
mapokezi na anaamini mchango wake katika soka la Tanzania unahitajika.
“Mustakabali wa mpira
wa miguu wa Tanzania utakuwa mkubwa kama Watanzania watapenda kufuatilia
masuala ya mpira wa miguu kupitia ligi tofauti tofauti, kadiri unavyoangalia
michezo mbalimbali ya kimataifa, ndivyo unavyozidi kujifunza” alisema Kanu.
Kanu alifanyiwa
upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo
inayoitwa “The Kanu Heart Foundation.”
Kanu mbali na kuchezea
timu yake ya Taifa, pia aliwahi kuchezea vilabu vya Iwuanyanwu Nationale kati
ya mwaka 1992 hadi 1993, mwaka 1993 hadi 1996 alichezea
AFC Ajax, mwaka 1996 hadi 1999 alichezea Inter Milan, mwaka 1999 hadi 2004
aliichezea Arsenal, mwaka 2004 hadi 2006 alichezea West Bromwich Albion na mwaka 2006 hadi 2012 alichezea
Portsmouth.
No comments:
Post a Comment