TANGAZO


Saturday, March 5, 2016

Wakimbizi na wahamiaji wafurika Ugiriki


  
Ugiriki
Kamishna wa Jumuiya ya Ulaya wa maswala ya wahamiaji amesema kuwa Ugiriki imefurika na wakimbizi na wahamiaji.
Dimitris Avramopolous ametoa wito kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo ya Ulaya kusaidia katika kusuluhisha hali hiyo badala ya kuiachia Ugiriki au Italia pekee.
Kati ya wahamiaji 2003 wanakisiwa kuingia Ugiriki kila siku.
Wengi wao hawawezi kusonga mbele kwa sababu ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Austria na mataifa ya Balkan.
Wahamiaji wanaoingia Ugiriki
Mwandishi wa BBC anasema kuwa matamshi ya Bwana Avromopolous ni ishara kuwa kiongozi huyo wa wahamiaji katika Jumuiya hana nia ya taifa lake kuzuiliwa kuwa mwanachama wa muungano wa paspoti wa Schengen.
Kwa kawaida mtu ye yote aliye na paspoti ya Schengen ana uhuru wa kusafiri bila vikwazo kwa mataifa mengine wanachama wa muungano huo.

No comments:

Post a Comment