Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwenyekiti wa umoja huo Seleman Kirungi na kusho ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (mwenye miwani) akisikiliza maelezo
kuhusu mwandishi wa Fasihi Hayati Sheikh Amri Abeid Kaluta kutoka kwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni _Sehemu ya Lugha Bibi. Shani
Kitogo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo
jijini Dar es Salaam.
Msherehesaji katika hafla ya uzinduzi wa Umoja
wa Washairi Tanzania (UWASHATA) Mfaume Rashid akisisitiza jambo wakati wa zoezi
la uzinduzi wa umoja huo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha,Mlezi mstaafu wa
UKUTA Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu na mwakilishi wa UWASHATA Charles
Mloka
Mjukuu wa Hayati Mathias Mnyampala Bw. Stanley
Machichimi Mnyampala akimpa zawadi ya Kitabu cha fasihiNaibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho kinajulikana kwa jina la “Maisha Gharamia” ambacho kilitungwa na Babu
yake.Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta
Mosha,Mlezi mstaafu wa UKUTA Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu na mwakilishi
wa UWASHATA Charles Mloka.
Mtoto wa Hayati Amri Abeid Kaluta akimkabidhi
zawadiya kitabu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi
Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kinajulikana kwa
jina la “Maisha Gharamia” ambacho
kilitungwa na Babu yake. Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI)
Dkt. Ernesta Mosha,Mlezi mstaafu wa UKUTA Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu
na mwakilishi wa UWASHATA Tawi la Dodoma Charles Mloka.
Mmoja wa wasanii wa Ushairi akielezea namna
Kitabu cha “Kivuli cha Mvumo” wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja huo leo
jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha,Mlezi mstaafu wa UKUTA Prof Mulokozi na
Mwandishi wa vitabu na mwakilishi wa UWASHATA Charles Mloka.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa na Mweyenyekiti wakiwa wameshika Hati
ya usajili wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Umoja huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa umoja huo Seleman
Kirungi na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI)
Dkt. Ernesta Mosha.
Msherehesaji katika hafla ya uzinduzi wa Umoja
wa Washairi Tanzania (UWASHATA) ambaye pia ni ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Kampuni za Mfaume Rashid akionyesha moja ya vitabu alivyo vitunga leo wakati wa
hafla ya uzinduzi wa huo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huo leo. Vitabu
hivyo ni pamoja ma Kivuli cha Kiamboni, Umbuji wa Kiswahili na Nuru Gizani.
Baadhi ya Wafanyakazi
kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakiangalia tarifa mbalimbali kuhusu
waandishi wa vitabu vya Fasihi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi
Tanzania (UWASHATA).
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanachama wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Umoja huo leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija,WHUSM)
No comments:
Post a Comment