Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo dhidi ya Mbeya City, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 2-0 na hivyo kuongoza msimamo wa ligi hiyo, baada ya Yanga na Azam zilizokuwa zikiongoza msimamo wa ligi hiyo, kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wao waliocheza jana uwanjani hapo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mchezaji Mohamed Hussein (kulia) wa Simba akipiga mpira krosi kuelekea langoni mwa Mbeya City wakati wa mchezo huo, huku akikabiliwa na Hassan Mwasapila wa Mbeya City.
Wachezaji wa Simba na Mbeya City wakiwania mpira wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia timu yao wakati wa mchezo huo.
Ibrahim Ajib wa Simba akiwa amedondoka nchini wakati akiwania mpira na Tumba Suedi (15) wa Mbeya City.
Danny Lyanga wa Simba akikokota mpira huku akifuatwa na Tumba Suedi wa Mbeya City.
Mwinyi Kazimoto wa Simba akijaribu kumpiga chenga Joseph Mahundi wa Mbeya City wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Simba, Danny Lyanga (kushoto) na Awadhi Juma wakipongezana huku mashabiki wa timu hiyo, wakifurahia baada ya Danny Lyanga kuifungia timu yake hiyo, bao la kwanza katika mchezo huo.
Ibrahim Ajib akikimbia kushangilia bao hilo baada ya yeye na mwenzake kufanya kazi ya ziada kuifungia timu yao bao la kwanza katika mchezo huo.
Awadhi Juma (kushoto) na Ibrahim Ajib, Ajibu akishangilia baada ya kuipatia bao la kwanza timu yao ya Simba wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Simba Dyanny Lyanga na Awadhi Jumaa wakishangilia bao hilo.
Dyanny Lyanga akijaribu kumtoka Tumba Suedi wa Mbeya City.
Danny Langa akiudibiti mpira huku akifuatwa na Tumba Suedi wakati wa mchezo kati ya timu hizo jana.
Danny Langa akiudibiti mpira huku akifuatwa na Tumba Suedi wakati wa mchezo kati ya timu hizo jana.
Joseph Mahundi wa Mbeya City akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa pia na Hassan Kessy wa Simba.
Ibrahim Ajib wa Simba (kulia), akijaribu kumpiga chenga Haruna Shmte wa Mbeya.
Ibrahim Ajib wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Haruna Shmte wa Mbeya.
Ibrahim Ajib wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Haruna Shmte wa Mbeya.
Wachezaji wa Simba, Awadhi Juma (kushoto), Ibrahim Ajib aliyepiga magoti na Danny Lyanga wakishangilia bao la pili la timu hiyo, lililofungwa na Ibrahim Ajibu wa Simba.
Wachezaji wa Simba, Awadhi Juma (kushoto), Danny Lyanga (katikati) na Ibrahim Ajib (kulia), wakishangilia ndani ya nyavu za lango la Mbeya City baada ya Ajib kuifungia bao la pili timu yake ya Simba katika mchezo huo.
Mlinda lango wa Mbeya City akiwa ameduwaa baada ya Ibrahim Ajib kufunga bao la pili kwa timu yake ya Simba wakati wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment