Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kifalme ya Norway, Tone Skogen akizungumza wakati
wa ufuzinduzi wa mpango wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini Dar es Salaam leo. Serikali ya nchi hiyo imetoa Dolla za Kimarekani milioni 5 kwa ajili ya uboreshaji huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa mkutano wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kwenye uzinduzi wa mpango wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kifalme ya Norway, Tone Skogen.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika uzinduzi wa mpango huo, wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, kati ya Serikali ya Tanzania na Norway, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Maofisa wa TRA na wa Wizara ya Fedha wakiwa katika mkutano huo, wa pamoja katika ya Serikali ya Tanzania na Norway katika uzinduzi wa mpango wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, jijini Dar es Salaam leo.

Waandishi wa habari, wakichukua habari, wakati wa uzinduzi wa mpango huo, wa ushirikiano wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, kati ya Serikali ya Tanzania na Norway, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo, wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kwenye uzinduzi wa mpango wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, jijini Dar es Salaam leo. Serikali ya Norway imetoa Dolla za Kimarekani milioni 5 kwa ajili ya uboreshaji huo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Tone Skogen.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa uzinduzi wa mpango wa kuboresha ukusanyaji kodi nchini, jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, akitoa ufafanuzi kwa wandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kifalme ya Norway, Tone Skogen.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kifalme ya Norway, Tone Skogen (kulia), Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (wa pili kushoto) na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (wa pili kulia), wakizungumza jambo wakati wa mkutano huo.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
10/03/2016
Dar es Salaam
SERIKALI ya Kifalme ya
Norway imetoa kiasi cha Dolla za kimarekani milioni 5 kwa Serikali ya
Tanzania kwa kuwaunga mkono Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya
awamu ya tano katika jitihada zake katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato
nchini.
Makubaliano hayo ya
ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Naibu
Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja
na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.
Akizungumza katika ufunguzi
huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone
Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuimarisha na kuongeza kodi ya
mapato ya ndani kwa kuhakikisha kwamba mianya
ya wakwepaji kodi inazuiwa.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali
imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi
bila kushurutishwa ili kuondokana bajeti
tegemezi kutoka nje.
“Lengo la kuimarisha uelewa
wa wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji
kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na
kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji
wa mapato nchini” alisisitiza Naibu
Waziri huyo.
Naye Kaimu Kamishna Mkuu TRA
Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo
wa wataalamu nchini kwa kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika
makampuni makubwa nchini.
Awali Serikali ya Kifalme
ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani million 3 katika mpango huo wa
kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

No comments:
Post a Comment