Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika nje ya chuo ya Illinois saa chache kabla ya bwana Trump kuwasili.Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri.
Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi.
Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.

No comments:
Post a Comment