Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani Mitt Romney amesema kuwa atampigia kura seneta wa Texas Ted Cruz kwa kuwa ''havutiwi'' na mgombea wa chama hicho aliye kifua mbele Donald Trump.
Bwana Romney amesema katika mtandao wake wa facebook kwamba njia ya kipekee ya kumchagua mgombea wa Republican ni kupitia mkutano ambapo wanachama wanamchagua atakayegombea kupitia chama hicho.
Donald Trump na Mitt Romney
Alifanya kampeni na Gavana John Kasich huko Ohio lakini akasema kuwa kumpigia kura Bwana Cruz ndio nijia ya kipekee kumzuia Trump.
Anajiunga na viongozi wengine wa Republican wanaomuunga mkono Bwana Cruz. Ted Cruz
Bwana Trump ameshinda majimbo mengi na kwa sasa ana takriban wajumbe 678 huku akitakiwa kujipatia wajumbe 1237 kushinda uteuzi huo.
No comments:
Post a Comment