Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Luis Inacio Lula da Silva, amekubali cheo cha uwaziri ndani ya serikali ya Dilma Rousseff.
Wanachama wa chama cha wafanyikazi wamesema kuwa uteuzi huo utaupa nguvu utawala wake unaolegea.Akiwa waziri Lula atakuwa na haki ya kinga.Wiki iliopita waendesha mashtaka walitaka akamatwe kutokana na uchunguzi wa ulanguzi wa fedha wa jumba moja la kifahari lililopo katika ufukwe wa bahari.
Rais huyo wa zamani aliye na umaarufu mkubwa amekana kufanya makosa yoyote na kusema kuwa madai hayo yanashinikizwa kisiasa.
Lula alizuiliwa kwa mda mapema mwezi huu baada ya uchunguzi kusema kuwa kuna ushahidi alipokea faida katika mpango ulioshirikisha kampuni ya mafuta ya Petrobras.

No comments:
Post a Comment