Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja mechi ya Alhamisi ya kombe la Europa kati ya Liverpool na Manchster United kuwa mechi kubwa sana.
Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.Hatahivyo Klopp anasema :''kila siku kombe la Europa linafurahisha.Ni Mechi kubwa sana.Ijapokuwa sio kubwa zaidi katika kazi yangu kama mkufunzi wa Liverpool lakini ni muhimu sana''.
Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.

No comments:
Post a Comment