TANGAZO


Friday, March 11, 2016

Korea Kaskazini yaamrisha majaribo zaidi ya mabomu


 
rais Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ameamrisha majaribio zaidi ya kinyukilia yakitumia mabomu yasiyokuwa na nguvu, ambayo anasema wanasayansi wa nchi yake wametengeneza.
Shirika la utangazaji nchini limetangaza kwamba Kim alitoa amri hiyo baada ya kushuhudia uzinduzi wa makombora mengine hapo Alhamisi.
Awali kiongozi huyo alisema wanasayansi wa nchi yake wamefanikiwa kupunguza ukubwa wa mabomu ili yaweze kuwekwa kwenye makombora.
Korea Kaskazini
Waandishi wa habari wamesema ikiwa hili litathibitishwa, hii itakua tishio kubwa kwa Korea Kusini na nchi nyingine zilizoko kwenye kanda hiyo.

No comments:

Post a Comment