Na Magreth Kinabo-MAELEZO
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa msisitizo, kwa halimashauri, viongozi wa dini na watu mashuhuri wasaidie kutoa elimu sahihi juu ugonjwa wa kipindupindu ili iweze kuacha imani potofu kuhusu sababu mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huo.
Aidha wizara hiyo imesema kwamba udhibiti wa ugonjwa huo ni lazima uwe endelevu na ushirikishe viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya chini ya kijiji kwa kushirikisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii,Serikali za mitaa,afisa watendaji hadi ngazi ya wilaya na mkoa kwa kuwa unasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa kwenye baadhi mikoa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,John Michael wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dares Salaam.
“Kuhakikisha kuwa jamii ina uelewa wa kupata matibabu mapema katika vituo vya kutolea huduma.
Aidha mikoa pamoja na halimshauri ihakikishe upatikanaji wa chumvi chumvi za kuweka kwenye maji(ORS).Hii ikiwa ni moja ya matibabu ya awali ambapo mgonjwa mwenye dalili za kipindupindu anasisitizwa atumie maji yaliyochanganywa na ORS wakati anapelekwa katika kituo cha kutolea huduma.
“Tumeshuhudia vifo vingi vinatokea katika jamii kabla ya kufika kituo cha kutolea huduma ambavyo vingeepukika iwapo matumizi ya ORS katika ngazi ya jamii yangefanyika,” alisisitiza.
Aliyataja mambo ambayo yanaweza kusaidia kuwa ni upatikanaji wa maji safi na salama kupitia mamlaka za maji zilizopo katika ngazi zote, kuhakikisha utunzaji salama wa maji ya kunywa yaliyotibiwa na kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo yote ya mijini na vijijini ili kupunguza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huu.
Aliongeza kwamba kutokana na kudumu na kuongezeka kwa kasi ya ugonjwa huu hapa nchini wizara yangu imeweka mikakati zaidi ikiwa ni pamoja na kupeleka ombi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu la kutaka kuitisha mkutano wa kamati ya dharura ya taifa ambayo inajumuisha makatibu wakuu wote ili suala hili liweze kujadiliwa kitaifa kwa upana zaidi hasa kwa kuzingatia hali ya sasa ya mvua. Lengo ni kuimarisha mikakati ya pamoja ya kitaifa.
Kaimu Katibu Mkuu huyo aliongeza kwamba kwa mujibu wa takwimu za wiki iliyopita, kuanzia Machi 7 hadi Machi 13 2016 zinaonyesha kuwa ,kasi ya ugonjwa hu alisema idadi ya wagonjwa waliopotiwa wiki hiyo ni 758 ikilinganishwa na 544 wa wiki iliyotangualia Februari 28 hadi Machi 6, mwaka huu.
Aliitaja mikoa iliyoathirika na ugonjwa huo, Morogoro 196, Dodoma142, Mwanza,108, Mara 86, Manyara 77, Iringa 77, Dares Salaam 42, Mbeya, Mbeya, 16, Arusha 10 na Lindi 2, Mtwara 2 na Rukwa 2.


No comments:
Post a Comment