China imepiga marufuku meli za Korea kaskazini kuingia katika bandari zake kuanzia hivi leo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa china ameripotiwa kutangaza vikwazo hivyo katika mkutano wa kila mwaka wa maafisa wa chama cha kikomunisti mjini Beijing.Hatua hiyo inaileta China sambamba na vikwazo vikali vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini wiki iliyopita.
Siku ya Jumanne kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa nchi yake imeunda zana za kinuklia zinazoweza kutundikwa kwenye makombora ya masafa marefu.

No comments:
Post a Comment