Klabu ya Arsenal ya Uingereza itashuka ugani Nou Camp kwa mechi ya marudiano dhidi ya miamba wa Ulaya Barcelona, wakikabiliwa na kibarua kigumu katika juhudi za kutaka kufika robofainali.
Meneja wao Arsene Wenger amesema wachezaji wake wamejiandaa kucheza vyema na kwamba ni muhimu sana kwao kufunga.“Hatuhitajiki kufanya hesabu sana, tunajua ni lazima tushambulie na tufunge,” amesema Wenger.
“Wachezaji wameungana pamoja tayari kucheza vyema.”
Arsenal wanahitaji kufunga mabao mawili Nou Camp bila kufungwa bao jingine ndipo angalau wajipe matumaini ya kusonga.
Beki wa Arsenal Laurent Koscielny atarejea kuwaongeza nguvu baada ya kukaa nje kutokana na jeraha.
"Tumeshinda katika kila uwanja Ulaya lakini huko (Nou Camp) hatujafanikiwa bado,” anasema Wenger.
"Mtazamo wetu haukuwa mbaya lakini tuliteleza na tukaadhibiwa.
"Itatupa moyo sana kipindi kilichosalia cha msimu iwapo tutacheza vyema Jumatano.
"Huwa twapigana kushinda vikombe na kwa sasa hatupigiwi upatu kushinda msimu huu. Lakini bila kujali changamoto, Ligi ya Premia bado iko wazi na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya nafasi ni finyu sana.”

No comments:
Post a Comment