TANGAZO


Tuesday, March 8, 2016

Al-Shabab wakiri kushambuliwa na Marekani

Marekani Marekani imesema wapiganaji zaidi ya 150 waliuawa
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab nchini Somalia limethibitisha kwamba maeneo yake yalishambuliwa kwa mabomu na Marekani.
Wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema wapiganaji 150 wa al-Shabab waliuawa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Jumamosi katika kambi ya mazoezi ya wanamgambo hao.
“Marekani ilirusha mabomu katika eneo linalothibitiwa na al-Shabab. Lakini walitia chumvi kwenye idadi ya waliofariki. Hatuwezi kuwaweka pamoja wapiganaji 100 kwa sababu za kiusalama. Tunajua kumejaa ndege angani,” msemaji wa kundi hilo Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia Reuters.
Hata hivyo hakusema ni wapiganaji wangapi wa kundi hilo waliuawa.

No comments:

Post a Comment