Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habarileo jijini Dar es salaam
kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani. (Picha zote na Ally Daud, Maelezo)
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wanatarajia
kutoa elimu, huduma na vipimo vya bure vya magonjwa ya saratani ili kuiwezesha jamii
kujikinga na ugonjwa huo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
(Jumatano) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Ulisubisya Mpoki huduma hizo
za matibabu na vipimo vitaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya saratani
duniani inayoathimishwa ulimwenguni kote tarehe 4. Februari ya kila mwaka.
Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika
katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda
kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi
dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza
Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu
wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya
saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri
ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema
ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi
ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya
Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA
JANGA LA SARATANI DUNIANI.”
|
No comments:
Post a Comment