TANGAZO


Wednesday, February 3, 2016

Simba ilivyoikung'uta Mgambo FC mabao 5-1, Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo

Mashabiki wa  Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Mgambo FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 5-1. (PIcha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Hamis Kiiza akiwania mpira wa juu na Bakari Mtama wa Mgambo FC. 
Haji Ugando wa Simba akipiga mpira huku akifuatwa na Bakari Mtama wa Mgambo FC. 
Haji Ugando wa Simba akijaribu kumpiga chenga Sunday Magoja wa Mgambo FC. 
Ubao wa matokeo  ukionesha Simba 2 na Mgambo Shooting 0.
Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya mabao 5 yaliyofungwa na timu hiyo dhidi ya bao 1 la Mgambo Shooting.
Haji Ugando wa Simba akipambana na Bakari Mtama wa Mgambo Shooting. 
Ibrahim Ajib wa Simba akishangilia bao lake na Haji Ugando (kulia), aliloifungia timu yake kati ya mabao 5 yaliyofungwa na timu hiyo dhidi ya Mgambo Shooting
Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya mabao 5 waliyofunga dhidi ya Mgambo FC iliyopata bao 1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. 
Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 3 na Mgambo Shooting 0, kabla ya kupata bao la kufutia machozi na huku Simba ikiongeza tena mabao 2 na kuifanya kushinda kwa jumla ya mabao 5-1. 
Haji Ugando wa Simba, akimtoka golikipa wa timu ya Mgambo FC, Mudathir Khamis wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 5-1.

No comments:

Post a Comment