Pages

Saturday, January 9, 2016

Waziri Nape Nnauye avipongeza vyombo vya habari kwa kufanya kazi nzuri wakati wa uchaguzi mkuu

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda akiwahimiza wahariri wa vyombo vya Habari (hawapo pichani) kuhusu kutenda wajibu wao wakati wote wanapofanya kazi zao kwani uhuru waendana na wajibu leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na wamwisho ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-Maelezo, Zamaradi Kawawa. 
Mhariri Mkuu wa Gazeti la The Guardian Bw. Jesse Kwayu akichangia hoja wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye. Bw. Kwayu alimsihi Mhe. Nape kuzidi kuwa karibu na waandishi na pia zitungwe sheria zitakazo wawezesha waandishi wa habari kupata habari kwa urahisi na kufanyakazi yao ya kuhabarisha jamii. 
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Jamhuri Media Ltd Bw. Deodatus Balile akichangia hoja katika kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo. 
Mhariri wa Gazeti la the Citizen Bw. Peter Nyanje akichangia jambo wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongea na wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) leo hii jijini Dar es Salaam. Mhe Nape alivipongeza vyombo vya Habari kwa kufanya wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi mkuu na kuwahaidi kuwa Serikali itakuwa karibu nao sana na kuhimiza kuwa serikali ya awamu ya Tano itatunga sheria nzuri itakayo rahisisha utekelezaji wa majukumu yao.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw. Absalom Kibanda. Picha na Daudi Manongi-), Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo(WHUSM).

No comments:

Post a Comment