TANGAZO


Sunday, December 6, 2015

Wawili kati ya refarii 3 hutukanwa uwanjani


Image captionTakriban marefari 2 kati ya watatu hutukanwa na kubezwa wakisimamia mechi za kandanda BBC imebaini.

Takriban marefari 2 kati ya watatu hutukanwa na kubezwa wakisimamia mechi za kandanda BBC imebaini.
Utafiti uliochapishwa majuzi na kupatikana na BBC umebaini kuwa asilimia kubwa ya marefarii wanaosimamia mechi kote nchini Uingereza huvumilia matusi makali wanapokuwa uwanjani.

Image copyrightGetty
Image captionRefarii mmoja kati ya 5 anasema kuwa amewahi kuvamiwa na mashabiki au wachezaji.

Takriban marefarii 2,000 ambao husimamia mechi mashinani walishiriki katika utafiti huu ambao dhamira yake ni kuimarisha uhusiano kati ya marefarii wachezaji na mashabiki.
Aidha mpango huo unaoitwa 'Respect programme' unadhaminiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza.
Refarii mmoja kati ya 5 anasema kuwa amewahi kuvamiwa na mashabiki au wachezaji.

Image captionRefarii mmoja kati ya 5 anasema kuwa amewahi kuvamiwa na mashabiki au wachezaji.

''Hatuwezi laza damu kuhusiana na swala la usalama na heshima ya marefarii,Lazima tulitie maanani'' ripoti hiyo ya FA inasema.
'Licha ya matukio mengi ya matusi idadi ya marefarii ambao wamevamiwa na kujeruhiwa ingali chini na hivyo kuna haja ya kuingilia kati ilikuzima matukio kama hayo mara moja' Ripoti hiyo inaelezea.
"kati ya mechi millioni 1.2 zilizochezwa msimu uliopita,asilimia 1 % pekee ya marefarii ndio waliojeruhiwa baada ya kutoa maamuzi yanayoudhi mashabiki.
Hata hivyo Daktari Jamie Cleland kutoka chuo kikuu cha Loughborough,mmoja kati ya walioendesha utafiti huo anasema ''Licha ya idadi hiyo kuwa ndogo,sharti FA ishughulikie swala la usalama na tabia za mashabiki na wachezaji wenye hasira za haraka la sivyo watu wengi zaidi wataogopa kuwa waamuzi katika mechi za kandanda.

Image copyrightAFP
Image captionKatika msimu uliopita wa 2014-15 matukio 100 ya kupigwa yaliripotiwa .

Watafiti wa vyuo vikuu vya ,Loughborough, Portsmouth na Edge Hill waliwahoji marefarii 2,026 England, Kisiwa cha Isle of Man, Jersey na Guernsey.
Refarii Donald Distin ni mmoja kati ya wale waliopigwa.
Distin mwenyeji wa Devon, ambaye ameamua mechi kwa kipindi cha miaka 15 alipigwa na mchezaji baada ya kumuonesha kadi nyekundu.
''Nilishukia nimezabwa makonde mazitimazito nikajipata nimeanguka chini '' Distin aliiambia BBC kuhusu tukio hilo mwaka uliopita.

Image copyrightAFP
Image captionTakriban matukio 374 ya ukosefu wa heshima yaliripotiwa hii ikimaanishwa kuburutwa kusukumwa na matusi makali.

''Niliumia kuanzia usoni hadi shingoni na hata nilihisi maumivu makali kifuani.''Macho yangu yaliumia''
Mchezaji aliyepiga anatumikia kifungo kufuatia shambulizi hilo.
Katika msimu uliopita wa 2014-15 matukio 100 ya kupigwa yaliripotiwa .
Takriban matukio 374 ya ukosefu wa heshima yaliripotiwa hii ikimaanishwa kuburutwa kusukumwa na matusi makali.

No comments:

Post a Comment