TANGAZO


Tuesday, December 8, 2015

Oscar Pistorius apewa dhamana

Mahakama


Image captionMahakama ya rufaa ilimpata na hatua ya mauaji

Mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini Oscar Pistorius amepewa dhamana akisubiri kuhukumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake 2013.
Kikao cha kumhukumu kitaandaliwa Aprili 18 mwaka ujao.
Jaji Aubrey Ledwaba amesema hakuna hatari kwamba Pistorius anaweza kutoroka akipewa dhamana kwani alijiwasilisha mahakamani mwenyewe leo.
Bw Pistorius, mwenye umri wa miaka 28, ametakiwa kulipa rand 10,000 ($700, £450) kama dhamana.
Ataendelea kutumikia kifungo cha nyumbani na atakuwa na kifaa cha kumfuatilia kielektroniki. Anaruhusiwa kuondoka nyumbani kati ya saa moja asubuhi hadi saa sita mchana katika eneo la nusu kipenyo la kilomita 20 kutoka kwa nyumba anamoishi.
Pistorius pia ametakiwa kusalimisha pasipoti yake kwa mahakama.
Anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 15, ingawa jaji huenda akampunguzia hukumu.
Bingwa huyo wa Olimpiki alirejea kortini leo baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini wa kumpata na hatia ya kuua bila kukusudia na badala yake ikaagiza ahukumiwe kwa mauaji.
Alikiri kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013 lakini akasema alidhani ni mwizi aliyekuwa ameingia nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment