Rais Barack Obama amelihutubia taifa la Marekani kufuatia shambulio la risasi la wiki iliyopita katika jimbo la California ambalo lilisababisha vifo vya watu 14.
Rais Obama amesema wazi kwamba hakuna ushahidi kwamba muuaji alikuwa anatekeleza mauaji hayo kwa maelekezo ya kundi lolote kutoka nje ya Marekani .
Huku akisisitiza kusema kwamba lilikuwa ni shambulio la kigaidi hivyo ni muhimu kupambana nalo, na suala hili lisionekane kama ni vita baina ya Marekani na waislamu bali ni kwa waislamu weye itikadi kali za kigaidi.
No comments:
Post a Comment