Takriban maafisa 20 wa kijeshi wamekamatwa nchini Burkina Faso baada ya serikali kutibua njama ya kumuachilia huru kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Septemba.
Maafisa mjini Ouagadougou wanasema kuwa serikali ilitibua njama ya kumuachilia huru jenerali Gilbert Diendere.
Vyanzo vya afisi ya waziri mkuu Isaac Zida vinasema kuwa , maafisa hao walikuwa na nia ya kuwaachilia huru washukiwa wote wa mapinduzi mbali na kukirejesha kikosi hicho cha kumlinda rais kilichopigwa marufuku kufuatia jaribio hilo la mapinduzi.
- Jenerali Diendere alishatakiwa mwezi Oktoba kwa kutekeleza jaribio hilo la mapinduzi.
Aliachia madaraka baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa umma na viongozi wa kikanda.
Kikosi chake kilichokuwa kikimlinda rais kimehusishwa na njama hiyo mbali na madai mengine mengi ya ukiukaji wa sheria na kwa ukatili uliotekelezwa wakati wa utawala wa rais Compaoré.
Njama hiyo imetibuka katika siku ambayo taifa hilo linamtarajia rais mpya kuchukua hatamu leo.
- Waziri mkuuu wa zamani Roch Marc Christian Kabore anaapishwa hii leo baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita.
Rais huyo mpya Roch Marc Christian Kabore amesema kuwa ''sheria itafwata mkondo wake''
Waziri mkuu Zida amesema ''Tumewatia mbaroni ilikutoa ilani kuwa njama kama hiyo hainabudi ila kutibuka''
- Watu 57, ikiwa ni pamoja na mafisa 20 wa kitengo cha kumlinda urais, wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo la mwezi Septemba.
Jenerali Diendere na Compaore, wanakabiliwa na tuhuma za mauji ya rais wa zamani wa taifa hilo Thomas Sankara.
Wamekanusha madai dhidi yao.

No comments:
Post a Comment