Yohan Cabaye anaweka Palace kifua mbele baada ya kusaidiwa na Bolasie.
18:31 Crystal Palace 0-0 Southampton
Uwanjani Selhurst Park, Paulo Gazzaniga amefanya kazi ya ziada kuyaweka hai matumaini ya Saints kuondoka na alama ugenini. Palace wanashambulia vikali.
18:25 BAOOOO! Man City 1-0 Swansea
Mchezaji wa zamani wa Swansea Wilfried Bony anaadhibu waajiri wake wa zamani kwa kutumbukiza mpira wavuni akitumia kichwa baada ya kona kupigwa.
Image copyrightReuters
18:13 Man City 0-0 Swansea
Uwanjani Etihad vijana wa Alan Curtis Swansea ndio wanaopata nafasi kwanza. Wayne Routledge anachomoka na kuona goli lakini anazuiwa kufunga na kipa Joe Hart.
18:04 BAOOOOO! Sunderland 0-1 Watford
Watford wanaanza kwa kishindi, wakifunga bao kupitia Odion Ighalo.
18:00 MECHI NNE ZINAANZA
Crystal Palace v Southampton
Man City v Swansea
Sunderland v Watford
West Ham v Stoke
17:38 Norwich 1-1 Everton
Mechi yamalizika sare, Everton walitawala kipindi cha kwanza lakini Norwich wakaamka na kudhibiti kipindi cha pili.
17:35 Norwich 1-1 Everton
Mechi yaongezwa dakika tatu. Norwich wanazidi kushambulia Everton.
17:28 Norwich 1-1 Everton
Dakika ya 83, mambo bado sare Carrow Road. Kumbuka bao la Norwich lilifungwa na Wes Hoolahan.
17:23 Mechi kati ya Manchester City na Swansea City ni miongoni mwa mechi zitakazoanza saa kumi na mbili. Swansea walimfuta kocha Garry Monk wiki hii, na sasa wamo chini ya mkufunzi wa muda Alan Curtis.
Hawa hapa wachezaji wa timu zote mbili:
Manchester City XI: Hart, Sagna, Mangala, Otamendi, Clichy, Y Touré, Fernandinho, Jesús Navas, Silva, Sterling, Bony.
Benchi: Kolarov, Caballero, De Bruyne, Delph, Demichelis, Roberts, Iheanacho.
Swansea City XI: Fabianski, Rangel, Fernandez, Williams, Taylor, Britton, Cork, Routledge, Ki Sung-yueng, Sigurdsson, Ayew.
17:17 Dakika ya 71, Cameron Jerome wa Norwich anapoteza nafasi nzuri ya kufunga.
17:11 Kumbuka Mchezo kati ya Manchester City na Swansea City utatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC kupitia matangazo yake ya ulimwengu wa soka.
17:04 Mechi kati ya Norwich na Everton inaendelea Carrow Road, timu ziko sare. Everton walikuwa wanaondoka kwa bao lililofungwa na Romelu Lukaku dakika ya 15. Hilo ni bao la sita Lukaku kufunga mtawalia katika mechi EPL. Norwich wamesawazisha dakika ya 47 kupitia Wes Hoolahan.
No comments:
Post a Comment