Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi wa Chama wakati alipohudhuria katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) Zanzibar uliofanyika leo, Ofisi Kuu ya chama hicho, Kisiwandui Mjini Unguja. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa chama, wakati alipowasili Ofisi Kuu, Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar leo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa siku moja wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto), Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia), wakiwa katika mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar, uliofanyika leo, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akiendesha mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar uliofanyika leo, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja. Kushoto ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar (NEC) wakifuatilia kwa makini mkutano wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui chini ya Mwenyekiti wake, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar, wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo, katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.







No comments:
Post a Comment