Cristina Fernandez de Kirchner anayeondoka madarakani Argentina amesusia hafla ya kumkabidhi mamlaka mrithi wake Mauricio Macri.
Kiongozi huyo ametofautiana na mrithi wake kuhusu ni wapi hafla hiyo inafaa kuandaliwa.
Bi Fernandez aliwaaga raia kwenye mkutano mkubwa wa wafuasi wake jana ambapo alitoa hotuba yenye hisia tele hisia nje ya ikulu Jumatano.
Alivishutumu vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa kuipiga vita serikali yake ya mrengo wa kushoto.
Aliwahimiza raia kuandamana barabarani iwapo watahisi kusalitiwa na serikali mpya inayoegemea siasa za mrengo wa kati-kulia.
Bw Macri tayari amewasili katika majengo ya Bunge akifuata msafara wa polisi na wanajeshi wenye kupanda farasi. Msafara wake uliwapita mamia ya maelgu ya watu waliojitokeza katika barabara za mji mkuu Buenos Aires.
Atakula kiapo mbele ya wabunge mwendo was aa sita saa za Argentina.
Baada ya hotuba yake ya kwanza, atasafiri hadi ikulu ya rais ambako atapokezwa ishara na nembo za urais.
Bi Fernandez alikuwa amesisitiza shughuli ya kukabidhi madaraka ifanyike mbele ya Bunge, ambako chama chake kina wingi wa viti.
Alisema yeye pamoja na mumewe ambaye ni mtangulizi wake, Nestor Kirchner, walipokezwa ishara na nembo za urais huko na hivyo basi hilo linafaa kuendelezwa.
Bw Macri kwa upande wake anasema kwa mujibu wa itifaki, hafla ya kupokezwa mamlaka inafaa kufanyika ikulu ya rais, kama ilivyokuwa kabla ya 2003.
No comments:
Post a Comment