
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu katika Chuo pekee cha VETA cha Wilaya ya Makete.
Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wanafunzi wakati wa mafunzo kwa vitendo.
Mwenyekiti Bodi ya Vyuo vya Veta Nyanda za Juu Kusini na mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza katika Chuo cha Veta Makete, Kabaka Ndenda.
Baadhi ya wazazi wakiwa katika mahafali ya chuo hicho kushuhudia watoto wao wakihitimu.
Wazazi na mgeni rasmi wakitembelea katika majengo ya kujifunzia kwa vitendo.
Mkuu wa Chuo cha Veta, Makete Ramadhan Sebo akitoa nasaha kwa watoto wanaoingia mtaani kujiajiri.
Na Mwandishi wetu
WATANZANIA wametakiwa kuwapelewa watoto wao katika vyuo
mbalimbali vya ufundi stadi elimu inayo zalisha ajira nyingi kuliko vyuo vikuu
hapa nchini ili kuepukana na tatizo la ajira.
Inadaiwa kuwa watu wanaojiajiri ni wengi wanao toka katika
vyuo vya ufundi kuliko wanano maliza vyuo vikuu kutokana na wanao toka vyuo
vikuu wanategenea kuajiliwa huku wa vyuo vya ufundi wakijikita kujitengenezea
ajira na kuachana na utegemezi kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Veta
nyanda za juu inayo jumuisha mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe, Kabaka Ndenda,
juzi katika mahafari ya kwanza kwenye chuo pekee ya wilaya cha Veta Makete,
alisema kuwa vijana wengi wanao maliza
katika vyuo vya ufundi wanauhakika wa kujiajiri kuliko wanao enda vyuo vikuu.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiona ni bora kumpeleka
mtoto wake katika chuo kikuu kuliko kumpeleka katika vyuo vya ufundi, alisema
kuwa Tanzania kutokana na ulivyo mfumo wa ajira watoto ni bora wakapelekwa
katika vyuo vya ufundi ili kutengeneza ajira.
“Tanzania tulikataa mfumo wa mwalimu Nyerere wa ujamaa
tukataka ukabaila wakati hatuwezi kwenda nao ndio maana tunapata shida kupata
ajira, Tanzania bado hatujafika hatua ya kusoma vyuo vikuu na kupata ajira moja
kwa moja,” alisems Ndenda.
Alisema kuwa licha ya vijana hao wanao fuzu mafunzo kuweza
kujiajiri wanatakiwa kuhakikisha kuwa wakitoka hapo wanaenda kuunda vikundi ili
waweze kukopesheka.
Hata hivyo wanafunzi hao waliiomba serikali kuhakikisha kuwa
inawapa sapoti pale watakapo kuwa wameunda vikundi vyao na kuweza kujikwamua
kimaisha kwa kupata mikopo kutoka serikalini.
Mkuu wa chuo hicho Ramadhani Sebo alisema kuwa wanafunzi hao
wanaenda kuajirika licha ya kuwa na changamoto za vifaa vya kufundishia katika
baadhi ya fani zinazo fundishwa katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na katika
fani ya ufundi magari.
Alisema kuwa wanafunzi katika chuo hicho wamefanya mafunzo
kwa vitendo na wameiva vyakutosha kwenda kuingia katika kujiajiri katika ufundi
na kuanza kujitegemea.
Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa ambacho ni chapekee cha
wilaya Tanzania nzima na kuwa kilianza na kozi mbili na sasa kina kozi 4 huku
kikifundisha masomo mtamboka.
Alisema kuwa kutokana na kuto kuwa na mabweni chuo hicho
wanafunzi wake wamepanga mitaani na kuwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa
kumaliza chuo kutokan ana changamoto za kutoka mbali na kukutana na vishawishi.








No comments:
Post a Comment