Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.
Mabalozi walioteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini wakijitambulisha kwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume kwa mara ya pili baada ya kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza Mkoani Geita mnamo mwezi Julai 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akimwangalia mtoto mwenye kipaji, Zaynab Dotto mwenye umri wa miaka 10 akipiga danadana kwa umahiri jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kulia ni Mratibu wa Michezo ya Vijana wadogo Bw. Raymond Gweba na kushoto ni mama mzazi wa mtoto Zaynabu Bibi. Pili Said.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akitoa zawadi ya mpira kwa mwanasoka wakike kutoka shule ya msingi Kingugi walioshiriki katika tamasha la Live Your Goals linalo hamasisha mpira wa miguu wa wanawake jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati mwenye koti la bluu), katika picha ya pamoja na wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto), akisisitiza jambo jana alipokutana na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kuikabidhi bendera ya taifa kabla ya kwenda nchi mbalimbali za afrika kwa ajili ya mazoezi ya kujihimarisha kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia)
akikabidhi bendera ya taifa kwa naodha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 15 Bw. Issa Abdi jana katika Viwanja vya Karume kwa ajili ya
kwenda nchini Rwanda, Uganda na Kenya kupata ujuzi na mazoezi kabla ya
kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017
nchini Madagasca.
Na Genofeva Matemu - Maelezo
WATANZANIA wametakiwa
kuibua vipaji vya michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake kwani michezo ni afya, biashara na ajira
inayoheshimika katika jamii.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel jana wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa
wanawake lililoandaliwa na FIFA na kufanyika jana katika viwanja vya Karume Jijini
Dar es Salaam.
Prof Gabriel amesema
kuwa wazo la kuboresha michezo nchini linapaswa kuwekewa jitihada katika kila
Mkoa kwa kuwa na timu ya mpira wa wanawake ili kuweza kuchuja lulu
itakayotengenezwa na mikoa yote nchini hivyo kuinua vipaji vya michezo.
“Kama wazazi wote
nchini wataweza kutambua vipaji vya watoto wao, kuviheshimu na kuviendeleza
katika fani mbalilmbali ikiwemo michezo Tanzania itakua katika nafasi nzuri
katika mashindano mbalimbali ya michezo duniani” alisema Prof. Gabriel.
Akizungumza wakati wa
tamasha hilo Naodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake Twiga Stars
ambaye pia ni balozi wa tamasha la Live Your Goals Bibi. Sophia Edward amesema
kuwa tamasha la Live Your Goals limekua na muitikio mkubwa kwani wasichana
wapatao 400 wenye umri kati ya miaka 12 na kuendelea wameshiriki na kupatiwa
nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu.
Bibi. Edward amesema
kuwa tamasha lililofanyika jana katika viwanja vya Karume ni tamasha la pili
baada ya kufanya tamasha la kwanza Mkoani Geita mwezi Julai na kuendelea
kuhamashisha wanawake wote wenye vipaji nchini kujitokeza wanaposikia tamasha
la mpira wa miguu kwa wanawake linafanyika kwani matarajio ya FIFA ni kufikia
na kuibua vipaji vya wanawake nchini.
Naye Bibi. Pili Said
mzazi wa mwanamke mwanasoka mwenye umri wa miaka 10 amekiri kujaribu kuzima
ndoto ya mototo wake mara kadhaa baada ya kumzuia kucheza mpira wa miguu hivyo
kuwataka wazazi wote nchini kutafakari na kuheshimu ndoto za vijana wao ili
kuweza kutimiza azma zao.










No comments:
Post a Comment