Walimu zaidi ya 100 wa Wilaya ya Sengerema wakiwa wamefurika katika mlango wa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo baada ya kuandamana jana hadi ofisini kwake kudai malimbikizo yao. (Picha zote na Yosef Mhangwa)
Walimu zaidi ya 100 wa Wilaya ya Sengerema wakiwa wamefurika katika mlango wa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo baada ya kuandamana jana hadi ofisini kwake kudai malimbikizo yao.
Walimu zaidi ya 100 wa Wilaya ya Sengerema wakiwa wamefurika katika mlango wa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo baada ya kuandamana jana hadi ofisini kwake kudai malimbikizo yao.
Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, Babu Sanare akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kudhibiti walimu walioandamana kwenda kudai malipo yao wasiingie ndani kwa mkurugenzi.
Walimu zaidi ya 100 wa Wilaya ya Sengerema wakiwa wamefurika katika mlango wa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo baada ya kuandamana jana hadi ofisini kwake kudai malimbikizo yao.
Walimu zaidi ya 100 wa Wilaya ya Sengerema wakiwa wamefurika katika mlango wa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo baada ya kuandamana jana hadi ofisini kwake kudai malimbikizo yao.
Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, Babu Sanare akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kudhibiti walimu walioandamana kwenda kudai malipo yao wasiingie ndani kwa mkurugenzi.
Mkuu wa kituo cha Polisi (OCS) Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezo Makosa ya Jinai wa Wilaya, Nzumira Miraji (kulia), wakiwa wamesimama kwenye mlango wa Mkurugenzi wa wilaya hiyo kudhibiti walimu walioandamana kudai malipo yao wasiingie ndani.
Na Yosef Mhangwa, Sengerema.
28/11/2015
WALIMU zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza juzi Ijumaa waliandamana kwenda katika Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kudai malimbikizo yao yanayofikia sh.1.1 Bill.
Walimu hao walifurika katika Ofisi ya Mkurugenzi kuanzia saa 3.38 asubuhi hali iliyosababisha sintofahamu baada ya Kaimu mkurungezi Vicenti Bushaija kuondoka ofisini kwake kisha ofisi yake kulindwa na Askari Polisi waliosimama mlangoni.
Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya alifika katika ofisi hiyo akiwa ameambatana na askari polisi 12 waliokuwa wamevalia vifaa maalumu pamoja na silaha mbalimbali yakiwemo mabomu ya machozi na zile za moto kwa lengo la kuimarisha ulinzi.
Hatua ya Mkuu wa kituo cha polisi(OCS), Babu Sanare Kulinda Ofisi hiyo ni baada ya kutokea kutokuelewana baina ya uongozi wa chama cha walimu wilaya (CWT) na kaimu mkurungezi Bushaija baada ya kutaka kukutana na walimu 10 badala ya walimu wote waliokuwa wameandamana.
Bushaija aliondoka katika Ofisi hiyo kuwakwepa walimu ambao hata hivyo hakujua kama ndiye aliyekuwa anakaimu nafasi ya mkurungezi.
Ilivyokuwa
Baada ya walimu Kufika ofisi ya Mkurugenzi ,Viongozi wa CWT katibu Ruhumbika Francis na Mwenyekiti wake Ezekiel Nyagwaswa waliingia ndani kuonana na naye na baada ya muda mfupi walitoka nje kuwajulisha walimu ujumbe waliopewa na Mkurungezi.
Wakati viongozi hao wakizungumza na kaimu mkurugenzi,kadri muda ulivyozidi kwenda walimu walizidi kuongezeka huku baadhi yao wakionekana kuwapigia simu walimu wenzao waliokuwa hawajafika katika ofisi hizo.
Katibu baada ya Mazungumzo na Kaimu Mrugenzi aliwaambia walimu“Jamani walimu tumeonana na mkurugenzi,amesema mteuwe walimu kumi wakaonane nae,ndiyo kilichotokea”.
Walimu walimkatalia katibu wao wakidai hawawezi kuondoka eneo hilo hadi pale atakapokubali kuwasikiliza,ndipo kaimu mkurugenzi alitoka nje kuwaambia walimu watawanyike kwenda kazini,kabla ya kutoweka katika eneo hilo.
Baadaye Mkurugenzi alitoka nje,na kuwataka walimu kuondoka “Ondokeni kwanza kuwa hapa mmevunja utaratibu nataka mrudi kwenye vituo vyenu vya kazi,nimemaliza”na baadaye aliondoka eneo hilo huku walimu wakidai kwamba bila kusikilizwa wangelala nje ya ofisi hiyo..
Muda mfupi baadaye askari polisi wakiongozwa na mkuu wa kituo cha polisi Sengerema walifika katika ofisi hiyo,na kuweka ulinzi kwenye mlango wa Mkurugenzi.
“Nawaombeni alichokisema mkurugenzi,mtawanyike…hebu tuelewani tusiongee kama kicha..kama kuna tatizo lolote la kiofisi inatakiwa mteuwe wawakilishi wenu…..hamna kibali cha kujikusanya hapa….kama hamtaki kufuata utaratibu,kinachotakiwa ni kutawanyika tusiongee kama vichaa wote”alisema OCD aliyekuwa amesimama kwenye mlango wa mkurugenzi.
Ocs aliwataka kuondoka kabla hawajatumia nguvu huku akiwataka kama wameshindwa kuteua wajumbe kumbe basi wangekiona cha mtema kuni.
"Kama ni kutupiga mabomu watupige sisi hatujaja kufanya fujo hapa hatuna mapanga wala silaha yoyote,kama wanatupiga kwa haki mtupige..kwanini tuletewe askari bila fujo."
''Tulishakutana na mkurugenzi lakini hatupewi majibu ya uhakika...na kuna walimu tumekuwa tukitishwa tunapofuatilia madai yetu"alisikika mwalimu Paulina Barnabasi
Kauli hiyo ya OCS ilikataliwa na walimu hao waliokuwa wamekasarika wakidai hawezi kuondoka eneo hilo hadi paler mkurungezi atakapowasikiliza huku wengine wakiomba mkurugenzi alirudi ili wakutane ukumbini kueleza kero zao.
“Tulishawahi kuja kufuatilia…tuliwatuma viongozi wetu lakini hatua zinazochukuliwa za kushughulikia madai yetu”alisikika mwalimu mmoja.
Mwenyekiti wa CWT alijaribu kuwatuliza walimu hao ambao walisababisha shughuli za ofisi hizo kusimama ,bila mafanikio hadi pale walipokubaliana kuteuwa wajumbe 10 kwenda kuonana na mkurugenzi.
“Cha msingi mwajiri wetu amekataa kukutana na sisi..hebu tujengeni hoja,watu wa usalama wanatutaka tuondoke hapa..hebu tujadiliane”alisikika Mwenyekiti akijaribu kuwatuliza.
Kabla ya kutokea kutokuelewa na baina ya Mkurungezi huyo na walimu askari Polisi waliokuwa wamebeba mabomu ya machozi na silaha za moto walifika eneo hili kwa ajiri ya kuimalisha ulinzi zaidi.
Madai ya Walimu.
Katibu wa CWT Mwalimu Ruhumbika alisema,hatua ya walimu kufika katika ofisi ya Mkurungezi ni kutokana na madai ya muda mrefu ya malimbikizo ya mishahara,matibabu,posho za walimu wapy na matibabu yanayofikia kiasi cha sh.1.1 Bill.
Alisema malimbikizo hayo ni ya toka mwaka 2010 ambayo wakati serikali inahakiki ofisi ya mkurugenzi haikupeleka taarifa za walimu hao.
Aidha pia,alidai kuwa ,madai ya walimu kwa mkurungezi ni walimu 372 kutopandishwa madaraja kwa bajeti ya mwaka 2014/15 lakini hadi sasa hakuna hata mmoja aliyewahi daraja na licha ya baadhi yao kuwa barua za kupandishwa madaraja bado hawajabadilishiwa mishahara yao.
“Kuna zaidi ya walimu 40 bado hawajabadilishiwa mishahara na wengine licha ya kukidhi vigezo vya kupanda vyeo lakini hajapanda.Pia katika bajeti ya mwaka 2015/16 zaidi ya walimu 1,479 kati yao walimu 972 ni walimu waliofikia ukomo wao katika madaraja”alisema katibu.
Alisema mwaka huu zaidi ya walimu 25 wameshastaafu bila kupanda daraja na wengine zaidi ya 40 licha ya kukalibia kustafuu mwaka huu bado hawajabadilishiwa mishahara yao.
Kaimu Mkurungezi.
Waandishi wa habari waliamua kumfuata mkurugenzi aliyotoka nje kwa hasira,kisha kudai kwamba ,Jana walikuwa na kwenye kikao na walimu na kuzungumzia nao.
Alisema baada ya mazungumzo walikubalina kwamba walimu watulie wakati serikali ikiendelea kuyashughulikia.
"madai yao yanashughulikiwa,watalipwa,kwa maana hiyo jana tuliongea nao,sisi tunawashughulikia madai yao"alisema na Kuongeza.
"Nimewaambia tutazungumza na viongozi wao,nafikiri waandishi mnielewe,nayashughulikia madai yao,nimewashauri vizuri sasa hivi tuko katika kipindi cha mitihani,nimewaambia warudi kazini,nimetaka wawakilishi wao tu."
Hata hivyo alipouliza kiasi cha madai ya walimu alisema hana takwimu sahihi hadi kwenda kuangalia kumbukumbu za taarifa hizo kwenye ofisi yake.





No comments:
Post a Comment