Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa pongezi kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari, Maelezo. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Bw. Daniel Zenda na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi. (Picha zote na Frank Shija, Maelezo)
Frank Mvungi, MAELEZO
RAIS mteule wa
Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.
John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kushinda kiti cha Rais katika uchaguzi mkuu
ulifanyika oktoba 2015 ikiwa ni
kielelezo cha utendaji bora alionyesha katika kuwatumikia watanzania kupitia nyazifa
alizotumikia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu Chama cha
Mapinduzi (CCM) Bi Zainab Abdallah wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
uliolenga kumpongeza Rais mteule kwa
tiketi ya chama hicho.
“Akifafanua Bi
Zainab amesema kuwa Rais Mteule Dkt. John
Pombe Magufuli ameshinda kiti cha Urais kwa kuwa ndiye mtu pekee ambaye
watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze kuwaletea maendeleo kwa kuwa ni mchapa
kazi na ameonyesha kwa vitendo dhamira hiyo katika utumishi wake kwa miaka yote
iliyopita “alisisitiza Zainab.
Bi. Zainab amesema kuwa
Rais mteule Dkt. Magufuli anayo dhamira ya dhati yakuwaletea maendeleo
watanzania ndiyo sababu hata kauli mbiu yake ililisisitiza kuwa “hapa kazi tu” hivyo ni wajibu wetu kama
watanzania kusisitiza umoja na mshikamano na kuondoa tofauti zetu ili tufanye
kazi kwa bidii ili kujenga uchumi wa taifa.
Akizungumzia wasifu wa
Rais Mteule Dkt. Magufuli; Bi Zainab
amesema kuwa ni mtu mwenye uzalendo,mwadilifu,mchapa kazi, na ambaye
watanzania wote wanamkubali kuwa anao uwezo wa kuliongoza Taifa katika kipindi
hiki.
Kwa upande wa
Uchaguzi mkuu Zainab amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki hali iliyowapa nafasi watanzania kuchagua
viongozi wanaowataka na kupelekea chama
cha mapinduzi kuongoza katika uchaguzi huo
kutokana na utendaji madhubuti wa viongozi wa Chama na Serikali.
Pia Bi Zainab alitoa
wito kwa watanzania kudumisha amani na umoja wa Kitaifa ulioasisiwa na Viongozi
wa kwanza wa Taifa hili ili kufikia maendeleo ya Kweli.
Shirikisho la wanafunzi
wa vyuo vikuu Chama cha Mapinduzi
(CCM) limekuwa likihamasisha vijana
kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa.
No comments:
Post a Comment