TANGAZO


Tuesday, November 10, 2015

Viongozi wateule wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakutana na watumishi wote

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akifungua kikao kilichowakutanisha watumishi  wa Ofisi ya Rais-Utumishi, na Taasisi zake katika hafla fupi ya kuwapokea Katibu Mkuu mteule Bw. HAB Mkwizu (wapili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu mteule Bw. Tixon Nzunda (wapili kulia). 
Naibu Katibu Mkuu Bw. Tixon Nzunda, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla fupi, iliyowakutanisha watumishi wote. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu. 
Mkurugenzi  wa Idara ya Utawala katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Nyakimura M. Muhoji akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Rais-utumishi wakati wa hafla fupi ya kuwapokea viongozi walioteuliwa kuongoza Utumishi. 
Katibu Mkuu  wa Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akizungumza na na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla iliyowakutanisha watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi. 
Viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Menejimenti wakiwa katika picha ya pamoja. 
Viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi pamoja na watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili katika picha ya pamoja, Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Nzunda aliwahi kuwa Afisa katika Idara ya Ukuzaji Maadili. (Picha zote James Mwanamyoto, Afisa Habari, Ofisi ya Rais-Utumishi)

No comments:

Post a Comment