Viongozi wa Dini, Kiongozi wa Waislamu, Muft wa Bakwata, Sheikh Aboubakar Zubeir na Askofu wa KKKT na mwakilishi wa CCT, wakizungumza jambo wakati wakishuka kwenye jukwaa la kumwapishia Rais mpya Dk. John Magufuli, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo.
Na Laurence-MAELEZO-Dar es Salam
Viongozi
wa dini nchini wamemtaka Rais mpya wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuiongoza Tanzania kwa kufuata misingi
ya haki na utawala bora na kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa
miongoni mwa wananchi.
Viongozi
hao wametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kumuapisha
Rais wa Awamu ya Tano.
Katika
nahasa zake Mufti na Sheikh Mkuu wa
Tanzania Abubakar Zuberi amesema kuwa Mungu ndio kila kitu
katika maisha ya mwanadamu na ndiye mteuzi wa mambo yote aliyefanikisha kumpata Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Ameongeza
kuwa ni vema kumtanguliza Mungu katika kuwaongoza vema wananchi wa Tanzania ili
kufikia malengo ya kujiletea maendeleo.
Naye
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo amesema kuwa uongozi ni dhamana kama ambavyo watanzania
walivyomlilia Mungu ili awawezeshe kufanya uchaguzi wa amani na ndivyo Rais wa Awamu ya Tano analo jukumu kufanya
kazi zake akiongozwa na Mungu ili kuendelea kudumisha amani, upendo na
ushirikiano uliopo katika taifa.
Kwa
upande wa Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri la Tanzania Alex
Malasusa amesema kuwa amani ni tunda la roho ni vema Watanzania waendelee kuidumisha na viongozi
wakiongoza nchi kwa hofu ya Mungu.
No comments:
Post a Comment