TANGAZO


Tuesday, November 10, 2015

Vieira kocha mpya wa New York City

Image copyrightGetty
Image captionPatrick Vieira
Kiungo wa zamani wa timu za Arsenal na Manchester City, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya New York City.
Vieira mwenye umri wa miaka 39 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani.
Kocha huyu alikua anakifundisha kikosi cha vijana wa chini ya umri wa 21 cha Manchester City. Vieira ni miongoni mwa nyota wa timu ya taifa ya ufaransa waliotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998.
Vieira ataanza majukumu yake rasmi Januari 1, 2016 akiwa na kibarua cha kuingoza timu hiyo kufanya vizuri katika ligi ya Marekani.

No comments:

Post a Comment