TANGAZO


Friday, November 13, 2015

Ushindi wa chama cha Suu Kyi wathibitishwa

Suu Kyi

Image copyrightEPA
Image captionSuu Kyi awali alisema chama chake kikishinda atakuwa juu ya rais
Chama cha upinzani nchini Myanmar kimepata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili, maafisa wa uchaguzi wamesema.
Baada ya matokeo ya asilimia 80 ya viti vya ubunge kutangazwa, chama cha National League for Democracy chake Aung San Suu Kyi kimepata zaidi ya thuluthi mbili ya kura, kiwango ambacho kinahitajika kuwezesha chama kumteua rais.
Hata hivyo, robo ya viti vyote vya ubunge imetengewa jeshi, hii ikiwa na maana kwamba jeshi bado lina ushawishi.
Chini ya katiba ya Myanmar, Suu Kyi hawezi akawa rais kwa kuwa ana watoto ambao wana uraia wa Uingereza na mumewe alikuwa Mwingereza.
Lakini licha ya hili, uchaguzi huo umesifiwa kwani ndio wa kwanza huru nchini Myanmar, ambayo awali ilijulikana kama Burma, katika kipindi cha miaka 25.
Matokeo ya mwisho rasmi yanatarajiwa katika siku chache zijazo, na baadaye shughuli ya kumtafuta rais inatarajiwa kuanza Januari mwakani bunge litakapofunguliwa.
Thein SeinImage copyrightEPA
Image captionThein Sein ameahidi kukubali matokeo ya uchaguzi huo
Rais wa sasa Thein Sein tayari amesema ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo.
Chama tawala cha Union Solidarity Development Party (USDP), ambacho huungwa mkono na jeshi, kwa sasa kimepata 5% pekee ya viti.

No comments:

Post a Comment