TANGAZO


Wednesday, November 11, 2015

Urusi yakiri tatizo la dawa za kusisimua misuli


Image copyrightEPA
Image captionDawa za kusisimua misuli

Riadha ya Urusi ina tatizo na utumizi wa dawa za kulevya,lakini marufuku ya kutoshiriki katika michezo ya Olimpiki itawaadhibu wanariadha wasiotumia dawa hizo kulingana na katibu mkuu wa shirikisho la riadha nchini humo.
Ripoti ya tume ya kukabiliana na utumizi wa dawa hizo duniani imeishtumu Urusi kwa kuendesha mpango wa kukabiliana na dawa hizo unaodhaminiwa na serikali.
Mikhail Butov wa shirikisho la riadha nchini Urusi ameiambia BBC kwamba madai hayo 'sio mapya kwa kila mtu'.
Shirikisho la riadha duniani IAAF linatarajiwa kupiga kura kuhusu uwezekano wa kuiwekea vikwazo Urusi siku ya ijumaa.

Image copyrightEPA
Image captionRipoti ya dawa za kusisimua misuli

Mwenyekiti wa tume huru ya Wada Dick Pound amesema kuwa shirikisho la riadha nchini Urusi Araf,linafaa kupigwa marufuku katika mashindano ya kimataifa wakati alipotoa hotuba yake siku ya jumatatu ili kuandamana na uchapishaji wa ripoti hiyo.
Limetakiwa pia kujibu kufikia siku ya ijumaa,ambapo baraza la shirikisho la riadha duniani IAAF litaamua iwapo litaipiga marufuku Urusi kushiriki katika riadha ya kimataifa.
Huenda pia likainyima nchi hiyo kuandaa mashindano yoyote katika siku za baadaye,ikiwemo mashindano ya vijana ya dunia huko Kazan mwezi Julai.

No comments:

Post a Comment