TANGAZO


Monday, November 16, 2015

Ukosefu wa Ajira changamoto ya Dunia



Na Mwandishi wetu
UUKOSEFU wa ajira ni changamoto kubwa duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi, amani na utulivu.Tanzania, miongoni mwa nchi za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na uwezo wao.

Kutokana na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini.  Matokeo yake ni; kiwango cha umasikini kimeongezeka.

Sababu kuu zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
·         Kutokuwa na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.

·Vijana kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao, hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.

.Elimu duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweza kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi. Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani katika soko la ajira.

Kutokana na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii wanayoishi.

Kwa hiyo, #RecruitMe kwa makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua fursa mpya zilizopo katika soko la ajira. Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.

Lengo kuu la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli. #RecruitMe itakupatia ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.

Ili kupata huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu. Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.

No comments:

Post a Comment