TANGAZO


Tuesday, November 17, 2015

Ufaransa yalipua vituo zaidi vya IS Syria


Image copyrightECPAD
Image captionUfaransa yalipua vituo zaidi vya IS Syria

Polisi nchini Ufaransa wameendelea msako dhidi ya kundi la wajihadi wanaoshukiwa kutekelea mauaji yaliyotokea mjini Paris Ijumaa usiku.
Tayari wamevamia makao zaidi ya 100 huku wakiwaweka washukiwa katika kifungo cha nyumbani.

Image copyrightReuters
Image captionNdege kumi za kijeshi zimeharibu kabisa vituo kadhaa vya mafunzo ya wapiganaji hao katika mji wa Raqqa.

Vyombo vya usalama vimemtaja mzaliwa wa Ubelgiji Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26, kuwa mshukiwa mkuu.
Wachunguzi wanashuku kuwa ndiye aliyenusurika kifo pekee yake baada ya shambulizi hilo.

Image copyrightAP
Image captionRais Hollande anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri wa maswal ya nje wa Marekani John Kerry ambaye anazuru Paris leo.

Wakati hayo yakijiri, ndege za kivita za Ufaransa zimetekeleza mashambulio mapya na makali zaidi dhidi ya ngome ya Islamic State nchini Syria.
Mashambulizi hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo Jumanne.
Waziri wa ulinzi jijini Paris, amesema kuwa ndege kumi za kijeshi zimeharibu kabisa vituo kadhaa vya mafunzo ya wapiganaji hao katika mji wa Raqqa.

Image copyrightAFP
Image captionVyombo vya usalama vimemtaja mzaliwa wa Ubelgiji Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26, kuwa mshukiwa mkuu.

Wizara hiyo pia inasema kuwa mashambulio hayo yametekelezwa kwa ushirikiano na majeshi ya muungano chini ya Marekani.
Hapo jana Jumatatu, Rais Francois Hollande, aliahidi bunge la Ufaransa kuwa, jeshi la taifa hilo litalikabili vilivyo kundi la Islamic State bila huruma, ili kujibu mashambulio ya kigaidi ya Ijumaa, jijini Paris.
Rais Hollande anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri wa maswal ya nje wa Marekani John Kerry ambaye anazuru Paris leo.

No comments:

Post a Comment