Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi Muda mfupi baada ya Dkt. Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.Wengine waliomzunguka Rais Magufuli ni kutoka kushoto Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya,Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na Rais Joseph Kabila wa DRC.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimpongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Mke wa Rais Uhuru Kenyatta, Mke wa Rais Mama Janet Magufuli na kulia ni Mke wa Mhe. Raila Odinga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichoandaa Rais Magufuli kwa heshima ya wageni waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake kuwa Rais wa awamu ya tano.
No comments:
Post a Comment