TANGAZO


Tuesday, November 17, 2015

Putin:tukomeshe njia za ufadhili kwa IS


Image copyrightAP
Image captionRais wa Urusi, Vladmir Putin ametaka kuzuiwa kwa mianya ya ufadhili kwa IS

Viongozi wa mkutano wa G20 nchini Uturuki wamesema wanamipango ya kuweka nguvu zaidi kupambana na vitendo vya kigaidi hasa kwa kuvunja mianya ya ufadhili wa kifedha kwa makundi ya kigaidi, Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema njia hiyo inapewa kipaumbele.
''Suala la mapambano dhidi ya ugaidi ni moja kati ya maswala muhimu,hasa baada ya matukio mabaya kama utekaji nyara na vifo vilivyotokea nchini Ufaransa, kama tunavyoelewa na imekuwa ikizungumzwa kabla, kuwa njia za ufadhili wa fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi vikomeshwe,nimetoa mifano kwa taarifa tulizonazo kuhusu watu kutoka nchi mbalimbali wanaotoa ufadhili kwa wanamgambo wa IS, tumebaini kuwa ufadhili huu unatoka nchi 40 zikiwemo baadhi za G20''. Alieleza Putin.
Nae Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa mashambulizi ya Paris yalikuwa yakipangwa nchini Syria lakini yaliandaliwa nchini Ubelgiji.Wapelelezi wanashuku kuwa mtu aliyekuwa anasuka mipango hiyo ni Abdelhamid Abaaoud, mwenye miaka 27, mbelgiji mwenye asili ya morocco, anatoka katika wilaya ya Molenbeek.
Polisi nchini Ubelgiji wamewashutumu watuhumiwa wawili na wanamtafuta Salah Abdeslam, raia wa ufaransa aishie mjini Brussels ambaye nduguye anaaminika kuwa alijitoa muhanga mjini Paris.

No comments:

Post a Comment