TANGAZO


Sunday, November 8, 2015

Myanmar: Uchaguzi wa kwanza katika miaka 25

Image copyrightEPA
Image captionShughuli za upigaji kura zimeanzaa nchini Myanmar.
Vituo vya kupiga kura vimefungwa nchini Myanmar, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao utashuhudiwa kumalizika kwa nusu karne ya utawala wa kijeshi.
Taratibu za kuhesabu kura zitaanza hatimaye leo Jumapili.
Image copyrightBBC Chinese
Image captionZaidi ya watu milioni 30 walijiandikisha kupiga kura
Hata hivyo matokeo kamili yatatangazwa baada ya siku kadhaa kuanzia leo.
Wapigaji kura walijitokeza kwa wingi huku wengi wao wakionyesha moyo wa kujitolea, kwani foleni ndefu zilishuhudiwa huku raia wakiwa watulivu.
Chama cha mwanasiasa wa upinzani Aung San Suu Kyi cha National League for Democracy kinatarajiwa kupata idadi kubwa zaidi ya kura,hata hivyo huenda ikashindwa kuunda serikali, kwani jeshi lina hakikisho la asilimia 25 ya vitu Bungeni.
Image copyrightBBC Chinese
Image captionRobo ya viti vingali vimehifadhiwa kwa makamanda wa jeshi.
Zaidi ya watu milioni 30 walijiandikisha kupiga kura, huku milolongo mirefu ya ikishuhudiwa katika vituo vya kupigia kura.
Badhi ya watu wamezungumzia hisia zao huku wengi wakifurahia kupiga kura ya kidemokrasia.
Robo ya viti vingali vimehifadhiwa kwa makamanda wa jeshi.
Chama cha upinzani cha National League for Democracy, kikiongozwa na mwanasiasa wa kike - Aung San Suu Kyi -kinatarajiwa kushinda viti vingi Bungeni, lakini kinahitaji kutwaa zaidi ya thuluthi mbili ya kura zote ili kuhakikisha kuwa mgombea wake, amekinyakuwa kiti cha urais.
Wanaharakati wa utetezi wa haki za binadamu wametaja shughuli hizo za upigaji kura kama ulioharibika tayari.
Image copyrightBBC Chinese
Image captionRobo ya viti vingali vimehifadhiwa kwa makamanda wa jeshi.
Wamekosoa uhalali wa orodha ya wapigaji kura, ambao umewabagua maelfu ya waislamu.
Bi Suu Kyi alikabiliwa na wapigaji picha alipowasili kwa gari kupiga kura mjini Yangon.

No comments:

Post a Comment