TANGAZO


Friday, November 6, 2015

Mtoto mkimbizi akutanishwa na wazazi wake

Image captionAzam akutanishwa na wazazi wake Ujerumani
Kijana mmoja wa Syria ambaye kutoweka kwake hospitalini mjini Belgrade akiwa katika kambi ya wakimbizi barani Ulaya kulizua hisia kali miongoni mwa mitandao ya kijamii ameunganishwa tena na wazazi wake nchini Ujerumani.
Mwandishi wa BBC John Sweeny aliyeongoza utafutaji wa Azam mwenye umri wa miaka mitano alichapisha habari hizo katika mtandao wa twitter.
Azama alisafiri mbele ya wazazi wake na mjombaake na alijeruhiwa wakati wa safari hiyo.
Habari yake ilianzisha kampeni katika mitandao ya kijamii yenye alama ya reli FindAzam.Azama hakuwa pekee katika familia hiyo aliyejeruhiwa wakati wa safari hiyo kutoka Syria kuelekea Ulaya.
Image captionAzam ,katikati na mwandishi wa BBC Sweeney Kushoto na mjombaake kulia
Kukutanishwa kwake na familia yake siku ya Alhamisi kulifanyika katika hopositali moja ya Ujerumani ambapo babaake anatibiwa mguu wake uliovunjika wakati wa safari hiyo kupitia Ugiriki.
John Sweeney alikutana na Azam huko Serbia mnamo mwezi Septemba alipokuwa akitengeza makala kuhusu wakimbizi hao.
Mvulana huyo alikuwa akilia na uchungu mwingi kwa sababu gari moja lilimkanyaga alipokuwa usingizini ,na hivyobasi kuvunja taya lake.Lakini kabla ya kukamilisha matibabu mjini Belgrade,Azam alipotea na mjombaake.
Image captionPicha za Azam zilizosamabzwa katika mitandao ya kijamii ili kumtafuta
Kwa kipindi cha BBC Newsnight,Sweeney aliitafuta njia iliochukuliwa na wakimbizi hao ambayo Azam na mjombaake walitumia,akisafiri kutoka Serbia hadi Hamburg ambapo mtoto huyo hatimaye alipatikana na kundi moja la waandishi wa BBC baada ya usakaji mrefu uliohusisha utumizi wa mtandao wa kijamii.
Mjombaake ameiambia BBC kwamba kigae kiliingia katika jicho la Azam wakati wa mashambulizi mjini Damascus na aliagizwa na wazazi wa mvulana huyo kuelekea naye haraka Ujerumani ili kutibiwa.

No comments:

Post a Comment