TANGAZO


Sunday, November 8, 2015

Mshindi wa Jaymillions afungukia mafanikio yake

*Ajenga nyumba ya kisasa na kuishi na familia yake Goba
*Na yuko mbioni kufungua biashara zake
Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania (kushoto) akimwelezea Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kulia)alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam. 
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto)akisalimiana na Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo, Alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam. 
Nyumba ya Irene Mrema anayoishi na familia yake Goba jijini Dar es Salaam aliyomalizia kuijenga baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi Milioni 100 alichojishindia mwezi wa Nne kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania.


MMOJA wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa inaendeshwa na Vodacom Tanzania iliyomalizika mwezi Aprili mwaka huu Irene Mrema, amesema tangu aibuke na ushindi amepata mafanikio makubwa mojawapo ikiwa ni kuweza kujenga nyumba ya kuishi na familia yake maeneo ya Goba nje kidogo ya  jiji la Dar es Salaam.

“Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunikwamua kimaisha kupitia Jaymillion ya Vodacom kwa kuwa imeleta mafanikio makubwa katika maisha yangu na familia yangu kwa kuwa imetuwezesha kujenga na kumiliki nyumba nzuri ya kisasa ambayo tayari tumehamia pamoja na familia yangu”.Alisema.

Mbali na ujenzi wa nyumba hiyo Irene Mrema alieleza kuwa hivi anajipanga kufungua biashara  ambayo bado anaifikiria kwa fedha alizosalia ili kuwezesha kukuza kipato cha familia “Natarajia kufungua biashara katika siku za hivi karibuni kwa ajili ya kuniwezesha kijitegemea na kuongeza kipato cha familia”.

Aliishukuru kampuni hiyo  kwa kubuni promosheni zenye kuboresha maisha ya wateja wake na kuongeza kuwa fedha hizo alizoshinda zimeweza kusaidia katika mambo mbalimbali ya kijamii na akifungua biashara atatoa ajira kwa wafanyakazi ambao nao watanufaika na ushindi wake.

”Mafanikio haya ambayo yanaonekana kwangu kama ndoto ukimwelezea mtu anaweza akashindwa kuamini hususani wale ambao wanakuwa na dhana kuwa promosheni za makampuni kwa wateja kama ilivyokuwa Jaymillion ni za uongo lakini napenda kuwahakikishia  kwamba hakuna uongo,upendeleo wala kujuana bali ni  bahati ya mtu na akishinda anapewa fedha zake kama ilivyotokea kwangu”.Alisema Irene kwa furaha.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambaye alifanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya washindi wa promosheni hiyo alisema amefurahishwa na hatua aliyofikia mshindi huyo ya kupiga hatua ya kimaendeleo kimaisha.

“Kwetu Vodacom mafanikio haya ya mteja ni faraja kubwa kwa kuwa mbali na kutoa huduma bora na kubuni huduma za kurahisisha maisha ya wateja pia ni kufanya maisha ya wateja wetu kuwa murua kupitia promosheni zetu”.Alisema Nkurlu.

Alisema promosheni za kukwamua maisha ya wateja zikiwa na tija na kuleta mafanikio kwa wateja zinahamasisha kampuni kuendelea kubuni promosheni zingine ili ziweze kubadilisha maisha ya wateja wengi zaidi.

Alimalizia kwa kuwataka wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo na zitakazokuwepo katika siku za usoni.

No comments:

Post a Comment